IMF yatahadharisha kuhusu athari mbaya za kiuchumi za wimbi la pili la corona
(last modified 2020-07-17T02:41:40+00:00 )
Jul 17, 2020 02:41 UTC
  • IMF yatahadharisha kuhusu athari mbaya za kiuchumi za wimbi la pili la corona

Mkuu wa Mfuko wa Fedha Duniani (IMF) ametahadharisha kuhusu hasara za kiuchumi duniani zitakazosababishwa na wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.

Bi Kristalina Georgieva ametahadharisha kuwa,  licha ya kuwepo viasharia vya kuboreka hali ya kiuchumi duniani,  uchumi wa duniaungali unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukiwemo wa kuibuka wimbi la pili la maambukizi ya corona; na serikali zinapasa kuendelea na ratiba mipango yao ya kukabiliana na hali hii. 

Mkuu wa IMF amewatumia ujumbe Mawaziri wa Fedha wa nchi za kundi la G-2- katika kukaribia kikao chao kuwa:  shughuli za kiuchumi zinaimarika taratibu na mipango ya kifedha ya dola trilioni 11 ya kundi hilo na nchi nyingine zimesaidia uchumi wa dunia, hata hivyo hatari bado haijaondoka. Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulikadiria kupungua ukuaji uchumi duniani mwezi Juni mwaka huu wa 2020.   

Aghalabu ya nchi duniani zinakabiliwa na changamoto mbalimbali  za kiuchumi  zilizosababishwa na kuenea virusi vya corona.  Huko Marekani kwa kuzingatia kuenea maambukizi ya corona nchini humo na kuaga dunia watu zaidi ya 140,000 kwa maambukizi ya corona kulikosababisha pengo kubwa kati ya kupanda kwa gharama na kushuka kwa mapato, kuimefanya Marekani hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu kukabiliwa na nakisi ya bajeti ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini humo ya dola bilioni 864.  

Marekani inaongoza kwa kesi za corona duniani  

 

Tags