Marekani yazidi kujiimarisha kijeshi nchini Syria
(last modified Mon, 01 Mar 2021 06:50:09 GMT )
Mar 01, 2021 06:50 UTC
  • Marekani yazidi kujiimarisha kijeshi nchini Syria

Duru mbalimbali za Syria zimetangaza habari ya kuzidi wanajeshi magaidi wa Marekani, kujiimarisha ndani ya ardhi ya Syria. Duru hizo zimesema, msafara mwingine wa wanajeshi magaidi wa Marekani umevuka Iraq na kujizatiti katika viunga vya al Hasakah, huko kaskazini mashariki mwa Syria.

Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, jeshi la Marekani limendelea na uuvamizi wake haramu ndani ya ardhi ya nchi hiyo kwa kutuma zana mpya za kijeshi kutoke nchini Iraq.

Kwa mujibu w ripoti hiyo, msafara huo wa kijeshi wa Marekani ulikuwa na malori magari ya deraya na vifaru, vyote kwa pamoja ni vyombo 23 vya kijeshi.

Mara kwa mara wanajeshi vamizi wa Marekani wanapelekwa nchini Syria kwa madai ya kuimarisha nguvu zao katika maeneo wanayoyadhibiti licha ya serikali ya Syria kulalamikia vikali uvamizi wa mabeberu hao wa dunia.

Marekani inapoiba mafuta ya Syria mchana kweupe

 

Wanajeshi wa Marekani na Uturuki na magenge yao ya kigaidi, kwa muda mrefu wanayakalia kwa mabavu na kiharamu maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Syria. Mbali na kuiba utajiri wa mafuta wa maeneo hayo, wanafanya vitendo vya kigaidi pia dhidi ya wananchi wa kawaida na askari wa serikali na makundi yanayopambana na magaidi nchini humo.

Kwa mara chungu nzima serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza kuwa wanajeshi magaidi wa Marekani na wale wa Uturuki pamoja na magenge yao ya kigaidi lazima yatoke nchini humo na yaruhusu wananchi wenyewe wa Syria wajiaulie mustakbali wao.

Si hayo tu, lakini pia siku chache zilizopita, jeshi la Marekani kwa amri ya Rais Joe Biden lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kambi za makundi ya muqawama yanayopambana na magenge ya kigaidi katika mpaka wa Iraq na Syria.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), John F. Kirby alisema Biden ndiye aliyeidhina kufanywa shambulio hilo dhidi ya ngome za wanamuqawama wa harakati za kujitolea wananchi za Hashd al-Sha’abi, Kata'ib Hizbullah na Kata'ib Sayyid al-Shuhada mashariki mwa Syria.

Tags