Apr 14, 2021 02:35 UTC
  • Mahakama Kuu ya India yatengua sheria ya marufuku ya kubadili dini

Mahakama ya Juu ya India imetengua sheria inayowapiga marufuku raia wa nchi hiyo kubadili dini kutoka kwenye imanii ya Kihindu na kuingia kwenye Uislamu au ukristo. Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo imesema kuwa, sheria hiyo inapingana na katiba ya nchi.

Ripoti iliyoandikwa na gazeti la La Croix la Ufaransa kuhusu maudhui hiyo imesema kuwa, uamuzi huo wa Mahakama ya Juu ya India ni ushindi mkubwa kwa wafuasi wa dini za wachache nchini India hasa Waislamu na Wakristo.

Ripoti hiyo imesema kuwa, uamuzi wa Mahakama ya Juu ya India wa kukataa sheria hiyo iliyopasishwa na chama tawala cha Bharatiya Janata, umezifurahisha sana jamii za Waislamu na Wakristo wa nchi hiyo.

Taarifa ya mahakama hiyo imesema kuwa, Katiba ya India inawadhaminia raia wote uhuru wa kubadili dini, kuitekeleza na kuieneza.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi

Ripoti ya gazeti la La Croix la Ufaransa inasema majimbo 8 ya India yameweka sheria zinazotambua kitendo cha kuhama itikadi za Uhindu na kuelekea kwenye dini nyingine kuwa ni kosa la jinai. Ripoti hiyo imesema, kimsingi, sheria hizo zinalenga dini mbili za Uislamu na Ukristo.   

Sheria hizo zinawazuia Waislamu kuhubiri dini yao au kuoa wanawake wa Kihindu ambako sharti lake ni kubadili dini ya wanawake hao na kuwa Waislamu.

Tags