Wananchi wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel
(last modified Sun, 01 Dec 2024 04:13:24 GMT )
Dec 01, 2024 04:13 UTC
  • Wananchi wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel

Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la utawala haramu wa IIsrael katika Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara za kulaani mauaji ya umati na jinai zinazofanywa na utawala pandikizi wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wake wa kuokoa maisha ya raia.

Maandamano hayo ni muendelezo wa upinzani wa wananchi wa Morocco dhidi ya jinai za Israel huko katika Ukanda wa Gaza.

Wananchi wa Morocco wamekuwa wakifanya maandamano ya mara kwa mara katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Gaza.

Waandamanaji nchini Morocco wamelaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa kuwatesa kwa njaa, kuwazingira kila upande na kujaribu kuwahamisha kwa nguvu watu wa Ukanda wa Ghaza.

Kadhalika wananchi wa Moroco wanaishinikiza pia serikali ya Rabat kufuta makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Israel.