Makumi wauawa Nigeria katika mashambulio ya Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1213-makumi_wauawa_nigeria_katika_mashambulio_ya_boko_haram
Watu 30 wameuawa katika mashambulio mapya yaliyofanywa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram katika vijiji viwili vya kaskazini mwa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2016 03:38 UTC
  • Makumi wauawa Nigeria katika mashambulio ya Boko Haram

Watu 30 wameuawa katika mashambulio mapya yaliyofanywa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram katika vijiji viwili vya kaskazini mwa Nigeria.

Ripoti kutoka Kano zinaeleza kuwa mashambulio hayo mapya yamezidi kutilia shaka ahadi na madai ya Rais Muhammadu Buhari ya kulishinda na kuliangamiza kundi hilo la kigaidi.

Mustafa Karimba, mmoja wa wanaharakati wa kaskazini mwa Nigeria anayeshirikiana na jeshi katika mapambano na kundi la Boko Haram amesema, katika kipindi cha siku mbili zilizopita washambuliaji waliobeba silaha moto na baridi wamevishambulia vijiji vya maeneo ya mbali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Katika mashambulio hayo, wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram wameua raia 30 na kuwajeruhi makumi ya wengine pamoja na kupora mali za wanavijiji hao hususan mifugo ya ng'ombe.

Makumi ya watu wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa katika wiki za karibuni na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram katika jimbo la Borno huko kaskazini mshariki mwa Nigeria.

Hii ni katika hali ambayo mnamo mwezi Desemba mwaka jana Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari alitangaza kuwa kundi hilo limeshindwa na kupoteza uwezo na nguvu zake.../