Mar 19, 2017 16:30 UTC
  • Miripuko mitatu yaua watu kadhaa karibu na mji wa Maiduguri, Nigeria

Hali ya taharuki imeukumba mji wa Maiduguri, kufuatia miripuko mitatu ya kigaidi iliyotokea karibu na mji huo na kuua watu kadhaa na wengne kujeruhiwa.

Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa, miripuko hiyo ya kigaidi iliyotokea katika kijiji kimoja kilicho karibu na mji wa Maiduguri imeua watu wasiopungua wanne na kijeruhi wengine wanane.

Sehemu ya hujuma za kigaidi za wanachama wa Boko Haramu Nigeria

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo, ingawa viashiria vinaonyesha kuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram ndilo lililotekeleza shambulizi hilo.

Kabla ya hapo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alitangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kudhibiti ngome muhimu na ya mwisho ya wanachama wa kundi hilo. Kiongozi huyo pia aliahidi kumaliza harakati za kundi hilo kufikia mwishoni mwaka 2015.

Watu wakiwa amepatwa na tahayari kufuatia hujuma hizo

Hata hivyo kinyume na ahadi yake, gange la kigaidi la Boko Haram limeendelea kufanya mashambulizi ya kigaidi katika maeneo tofauti ya ndani na nje ya Nigeria na kusababisha mauaji ya watu wengi na maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. Hadi sasa maelfu ya watu wameuawa tangu kundi la Boko Haramu lilipoanzisha mashambulizi yake nchini Nigeria, mwaka 2009.

Tags