Jan 25, 2024 07:34 UTC
  • Gaza
    Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway amekemea mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na hali mbaya ya Ukanda wa Gaza katika nyanja zote za kibinadamu na kijamii na kusema: "Hali ya hivi sasa katika eneo hilo ni sawa na Jahanamu ya duniani."

Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka uliomalizika wa 2023, utawala wa Kizayuni wa Israel, ukisaidiwa na nchi za Magharibi hususan Marekani, umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina, huku kimya cha jamii ya kimataifa na jumuiya zinazodai kutetea haki za binadamu ukiutia kiburi zaidi utawala huo wa Kizayuni wa kuendeleza mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Espen Barth Eide, ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya Gaza baada ya siku 110 za vita katika eneo hilo na kusisitiza ulazima wa kusitishaji mapigano huko Gaza.

Espen Barth Eide

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua katika hali ya sasa ili kukomesha kabisa vita huko Gaza na kuongeza misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

Barth Eide ameongeza kuwa: Norway iko tayari kufanya mkutano wa kimataifa kuhusu ujenzi mpya wa Gaza.

Mwezi uliopita wa Novemba pia serikali ya Norway ilikuwa imetoa wito wa kusitishwa mapigano huko Gaza. Wakati huo, Waziri Mkuu wa Norway alisisitiza kwamba mashambulizi makali ya Israel katika eneo la Gaza ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za vita.

Wakati huo huo, taarifa ya mashirika ya kimataifa inasema, vita vya uharibifu vya Israel dhidi ya watu wa Gaza vimesababisha uharibifu wa 75% ya shule katika ukanda huo.

Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza jana kuwa, idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia 25,700 na idadi ya waliojeruhiwa ni 63,740.

Tags