Israel: Changamoto kubwa inayotukabili ni uwezo mkubwa wa Hizbullah unaoongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39733-israel_changamoto_kubwa_inayotukabili_ni_uwezo_mkubwa_wa_hizbullah_unaoongezeka
Gadi Eizenkot, mkuu wa majeshi ya utawala haramu wa Israel ameonyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya kuongezeka uwezo wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2018 12:01 UTC
  • Israel: Changamoto kubwa inayotukabili ni uwezo mkubwa wa Hizbullah unaoongezeka

Gadi Eizenkot, mkuu wa majeshi ya utawala haramu wa Israel ameonyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya kuongezeka uwezo wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Eizenkot aliyasema hayo jana usiku kupitia hotuba aliyoitoa katika eneo lililo karibu na mpaka wa Lebanon na kuongeza kuwa, kuna changamoto nyingi ambazo jeshi la Israel litakabiliana nazo kwa sababu Hizbullah inaendelea kuimarisha nguvu na uwezo wake.

Gadi Eizenkot, mkuu wa majeshi ya utawala haramu wa Israel 

Kadhalika Gadi Eizenkot sambamba na kuashiria uwepo wa kijeshi wa harakati hiyo katika eneo kama harakati yenye kubeba silaha na yenye uwezo mkubwa, amelitaka jeshi la utawala huo bandia kufanya juhudi za usiku na mchana kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni hatari tarajiwa ya Hizbullah. Kabla ya hapo utawala khabithi wa Israel na katika vita ulivyopigana mara mbili huko nyuma na harakati hiyo ya Hizbullah ulishindwa na wanamuqawama wa harakati hiyo na wale wa Ukanda wa Gaza, na hivyo kulazimika kurudi nyuma.

Askari wa Israel walipokuwa wakilia kama watoto katika vita ya siku 33 2006

Vita ya siku 33 kati ya jeshi la Israel na Hizbullah vilianza mwezi Julai 2006 na kumalizika tarehe 14 Agosti mwaka huo huo, ambapo Tel Aviv ilipata hasara kubwa na kulazimika kurudi nyuma.