Naim Qassem: Hizbullah iko tayari kujibu mashambulizi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i41707-naim_qassem_hizbullah_iko_tayari_kujibu_mashambulizi_ya_israel
Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, wanamapambano wa harakati hiyo wako tayari kukabiliana na shambulio lolote la kijeshi au chokochoko za utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 16, 2018 00:29 UTC
  • Naim Qassem: Hizbullah iko tayari kujibu mashambulizi ya Israel

Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, wanamapambano wa harakati hiyo wako tayari kukabiliana na shambulio lolote la kijeshi au chokochoko za utawala haramu wa Israel.

Sheikh Naim Qassem Hizbullah iko tayari kukabiliana na uchokozi wa Israel iwapo utawala huo utaamua kuchukua hatua yoyote ya kijinga.

Amesema Hizbullah kama harakati ya mapambano imetangaza mara kwa mara kwamba daima iko tayari kukabiliana na chokochoko za Israel na kujilinda kwa kutumia nyenzo zote. 

Wapiganaji wa Hizbullah

Hata hivyo Sheikh Naim Qassem amesema Hizbullah haitarajii kwamba utawala haramu wa Israel utaanzisha vita dhidi ya Lebanon katika kipindi cha sasa na kwamba haionekana kuwa, mazingira ya sasa yanairuhusu Israel kuchukua uamuzi wa kuingia vitani.

Utawala haramu wa Israel umeanzisha vita vitatu dhidi ya Lebanon katika kipindi cha mwaka 1982, 2000 na 2016. Utawala huo pia umefanya mauaji kadhaa ya kigaidi ya nchi Lebanon.