Jul 16, 2018 04:04 UTC
  • Askari usalama wa Saudia wafyatuliana risasi; 5 waaga dunia na kujeruhiwa

Askari usalam watano wa Saudi Arabia wamepoteza maisha na kujeruhiwa kufuatia kujiri mapigano baina ya askari hao katika kituo kimoja cha upekuzi katika mpaka wa Najran kusini mwa nchi hiyo.

Abdallah al Ashuri msemaji wa polisi katika eneo la Najran ameeleza kuwa Jumamosi usiku askari usalama mmoja wa Saudi Arabia aliwamiminia risasi wenzake na kuwaua watatu na kuwajeruhi wengine wawili. 

Wiki iliyopita pia mwanajeshi mmoja wa Saudia katika hospitali ya Mfalme Salman mjini Riyadh alifyatua risasi na kumjeruhi mtu mmoja. Hii ni katika hali ambayo kufuatia kuonyeshwa video ya wanajeshi wa Saudia katika mitandao ya kijamii wakilalamikia hali waliyonayo katika medani za vita kusini mwa nchi hiyo; Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesisitiza kuwa vikosi vyote khususan ambavyo vipo katika mipaka ya nchi hiyo na Yemen havina haki ya kurekodi picha yoyote.

Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia

Wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa siasa zinazotekelezwa na Muhammad bin Salman zimezidisha ukosefu wa amani nchini humo.  

 

Tags