Hizbullah: Israel itajuta iwapo itaivamia tena Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49898-hizbullah_israel_itajuta_iwapo_itaivamia_tena_lebanon
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeonesha mkanda wa video ikiutahadharisha utawala haramu wa Israel kwamba, utajuta iwapo utaivamia ardhi ya Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 02, 2018 00:11 UTC
  • Hizbullah: Israel itajuta iwapo itaivamia tena Lebanon

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeonesha mkanda wa video ikiutahadharisha utawala haramu wa Israel kwamba, utajuta iwapo utaivamia ardhi ya Lebanon.

Mkanda huo wa video unaonesha ramani ya picha zilizochukuliwa kwa satalaiti zinazofichua ramani ya vituo vya kistratijia vya Israel kama kambi za jeshi, makao makuu ya jeshi mjini Tel Aviv, viwanda vya kusafishia mafuta na kituo cha silaha za nyuklia cha Dimona.

Mkanda huo pia unawaonesha wapiganaji wa Hizbullah wakijitayarisha kufyatua makombora huku Katibu Mkuu wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah akisikika akisema: "Shambulizi lolote la Israel dhidi ya Lebanon litajibiwa."

Mkanda huo wa video umemalizia kwa kusisitiza kwamba: "Ukifanya mashambulizi utajutia."   

Sayyid Hassan Nasrullah

Mapema wiki hii kamanda mmoja wa jeshi la Israel aliitaka Tel Aviv kutekeleza sera eti ya "mauaji yenye malengo" akisisitiza kuwa, kuuliwa kwa kiongozi wa Hizbullah Hassan Narullah kutatoa pigo kubwa kwa harakati hiyo.

Itakumbukwa kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon iliundwa baada ya utawala haramu wa Israel kuvamia ardhi ya Lebanon na kukalia kwa mabavu maeneo ya kusini mwa nchi hiyo katika miaka ya 1980.