Wakazi wa mkoa wa al Hasakah Syria waanzisha mapambano ya kuwafukuza wanajeshi wa Marekani
(last modified Fri, 14 Feb 2020 02:40:08 GMT )
Feb 14, 2020 02:40 UTC
  • Wakazi wa mkoa wa al Hasakah Syria waanzisha mapambano ya kuwafukuza wanajeshi wa Marekani

Gavana wa mkoa wa al Hasakah nchini Syria amezitaja hatua za mapambano zilizochukuliwa na raia wa vijiji kadhaa vya mkoa huo dhidi ya wanajeshi wa Marekani kuwa ni kuanza kwa mapambano ya wananchi ya kuwafukuza wanajeshi vamizi wa Marekani huko Syria.

Jaiz al Hamoud al Musa Gavana wa mkoa wa al Hasakah unaopatikana kaskazini mashariki mwa Syria amesema kuwa wakazi wa vijiji kadhaa mkoani humo wameonyesha muqawama kwa lengo la kuwafukuza huko Syria wanajeshi vamizi wa Marekani. 

Jaiz al Hamoud al Musa, Gavana wa mkoa wa al Hasakah nchini Syria 

Wakazi wa maeneo ya kandokando mwa mji wa Qamishli katika mkoa wa al Hasakah juzi walichukua hatua kadhaa dhidi ya wanajeshi wa Marekani ikiwa ni pamoja na kuzuia kupita magari ya wanajeshi hao vamizi sambamba na kuyasababishia hasara. Wanajeshi wa Marekani aidha wamejibu hatua hizo za wakazi wa mkoa wa al Hasakah kwa kuwafyatulia risasi; ambapo raia mmoja ameuawa.  

Wananchi wa maeneo ya mkoa huo mara kwa mara wamekuwa wakidhihirisha upinzani wao kwa uwepo wa wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Syria. 

Tags