Hizbullah: Saudia inaiunga mkono Israel kukalia kwa mabavu Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i6517-hizbullah_saudia_inaiunga_mkono_israel_kukalia_kwa_mabavu_palestina
Afisa mwandamizi wa harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amelaani kile alichokitaja kuwa juhudi za utawala wa Aal-Saud za kukwamisha muqawama wa Wapalestina dhidi ya utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa serikali ya Saudi Arabia inaunga mkono hatua ya utawala huo wa Kizayuni kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 06, 2016 08:38 UTC
  • Hizbullah: Saudia inaiunga mkono Israel kukalia kwa mabavu Palestina

Afisa mwandamizi wa harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amelaani kile alichokitaja kuwa juhudi za utawala wa Aal-Saud za kukwamisha muqawama wa Wapalestina dhidi ya utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa serikali ya Saudi Arabia inaunga mkono hatua ya utawala huo wa Kizayuni kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Sheikh Naeem Qasim, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo katika mkutano na wanazuoni wa Kiislamu mjini Beirut unaojadili mikakati ya kuupa nguvu muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Sheikh Qasim amesema utawala wa Riyadh umekua ukitangaza wazi wazi kuunga mkono jitihada za utawala ghasibu wa Israel za kuhakikisha kuwa taifa la Palestina halipati haki ya kurejea katika ardhi zake zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Kadhalika Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ametoa wito kwa ulimwengu wa Kiislamu kuwa macho dhidi ya njama za maadui wao wakiongozwa na Marekani, Israel na makundi ya kitakfiri yanayoungwa mkono na utawala wa Aal-Saud haswa katika eneo hili la Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo afisa huyo mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amekosoa matamshi ya hivi karibuni ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel aliyedai kuwa miinuko ya Golan ya Syria ni milki ya utawala huo ghasibu na kwamba eneo hilo daima litakuwa sehemu isiyotenganishika na utawala huo.