Mar 28, 2024 06:58 UTC
  • Kaboni nyeusi; sio tu inachafua mazingira, lakini pia inasababisha ongezeko la joto duniani

Kaboni nyeusi imetajwa kusababisha ongezeko la joto kwa wati zisizopungua 0.6 kwa kila mita mraba moja katika uso wa dunia. Haya yamebainishwa na Mhadhiri wa masuala ya uhandisi wa mazingira katika Chuo Kikuu cha Istanbul Uturuki.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la Uturuki la Anadolu, Burcu Onat ameweka wazi athari nyingi za uzalishaji wa kaboni nyeusi kwa hewa ya sayari ya dunia na madhara yake kwa afya ya umma. Amesema, ingawa kwa kawaida haiainishwi miongoni mwa gesi chafuzi, kaboni nyeusi inayojulikana kama masizi inatambuliwa kama sababu muhimu katika mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya afya ya binadamu.

Onat ameongeza kubainisha kuwa: "Karibu nanogramu 3 za kaboni nyeusi ziligunduliwa katika gramu 1 ya theluji huko Antaktika." Uzalishaji huo hasa unatokana na vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuchomeka kusikokamilika kwa makaa ya mawe, mafuta ya dizeli, petroli na biomasi.

Takwimu kutoka Muungano wa Hali ya Hewa na Hewa Safi (CCAC) zinaonyesha kuwa karibu tani milioni 5.8 za kaboni nyeusi zilitolewa mwaka 2019, huku matumizi ya nishati majumbani yakichangia asilimia 43 ya uzalishaji wa kaboni nyeusi ulimwenguni.

Kaboni nyeusi na uchafuzi wa hali ya hewa 

Profesa Burcu Onat anasema: Kaboni dioksidi inashika nafasi ya kwanza kati ya gesi chafu zinazosababisha ongezeko la joto duniani,  methane ya pili, na nafasi ya tatu inachukuliwa na kaboni nyeusi. 

 

Tags