Waislamu India wapinga uchochezi wa Wahindu
Waislamu wa India wamefanya maandamano mjini New Delhi wakipinga vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na Wahindu wenye misimamo mikali.
Waandamanaji hao wametoa wito wa kukabiliana ipasavyo na Wahindu hao wenye misimamo mikali ili kuzuia machafuko na ghasia baina ya wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini India.
Shabnam Hashimi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa maandamano hayo amelaani matamshi ya kichochezi yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Rasilimali Watu wa serikali ya Undia dhidi ya Waislamu na ametoa wito wa kutimuliwa kazi waziri huyo.
Siku chache zilizopita Waziri wa Maendeleo ya Rasilimali Watu wa India, Ram Shankar Katheria alihutubia mkutano katika mji wa Agra katika jimbo la Uttar Pradesh akitangaza vita dhidi ya Waislamu. Waziri Ram Shankar alitoa matamshi hayo baada ya watu wasiojulikana kuua kiongozi mmoja wa kieneo.
mMatamshi hayo yasiyo ya kuwajibika yamelaaniwa na vyama mbalimbali vya siasa nchini India.