Takwimu za mauaji ya watu London zimezidi za mji wa New York, Marekani
(last modified Fri, 09 Aug 2019 06:32:31 GMT )
Aug 09, 2019 06:32 UTC
  • Takwimu za mauaji ya watu London zimezidi za mji wa New York, Marekani

Polisi ya London imetangaza kuwa, takwimu za mauaji yanayofanyika katika mji mkuu huo wa Uingereza zimezidi zile za mauaji yanayofanyika kila siku katika mji wa New York huko Marekani.

Taarifa iliyotolewa jana na polisi ya London imesema kuwa, idadi ya watu waliouawa katika mji wa London tangu mwezi Febuari mwaka 2018  ni kubwa zaidi ya wale waliouawa katika mji wa New York.

Ripoti hiyo imesema mauaji mengi zaidi katika jiji la London yanafanyika kwa kutumia visu. 

Afisa wa zamani wa polisi ya London anasema: Kupunguzwa idadi ya polisi katika jiji hilo kulikosababishwa na kupungua bajeti ya jeshi hilo ni miongoni mwa sababu kuu za ongezeko la mauaji na uhalifu unaoshuhudiwa mjini London. 

Ripoti zinasema jamii za watu wenye asili ya Somalia ndizo zinazolengwa zaidi na kufanyiwa ukatili japokuwa mashambulizi hayo hayafungamani na watu wa jamii au eneo makhsusi la mji huo. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ukatili na mashambulizi hayo yamezidisha wasiwasi kwa raia wa Uingereza. 

Visu vinatumiwa zaidi katika mauaji ya watu London

Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza yanaonesha kuwa, zaidi ya mabarobaro 17,500 wenye umri wa miaka 14 wa Uingereza hutembea na visu au silaha ya moto siku zote.  

Tags