Wanaharakati waandamana Chicago, Marekani kulaani hujuma za Israel, Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57431-wanaharakati_waandamana_chicago_marekani_kulaani_hujuma_za_israel_gaza
Makumi ya wanaharakati wamefanya maandamano katika mji wa Chicago jimboni Illinois nchini Marekani, kulaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa hivi karibuni na ndege za jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 22, 2019 23:08 UTC
  • Wanaharakati waandamana Chicago, Marekani kulaani hujuma za Israel, Gaza

Makumi ya wanaharakati wamefanya maandamano katika mji wa Chicago jimboni Illinois nchini Marekani, kulaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa hivi karibuni na ndege za jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao wameutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kama mtekelezaji wa mauaji ya kimbari. Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na jumbe zinazosema: "Komesha Mzingiro wa Gaza Sasa Hivi", na "Komesha Ugaidi wa Israel."

Waandamanaji wengine walikuwa wamebeba picha zinazoashiria ukatili wa jeshi la utawala huo haramu, huku wengine wakibeba picha za baadhi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyofanywa na jeshi la Israel wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa duru za hospitali katika Ukanda wa Gaza, kwa akali Wapalestina 30 waliuawa katika hujuma hizo zilizofanywa na ndege za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya eneo hilo ambalo liko chini ya mzingiro.

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba bendera ya Palestina

Katika hatua nyingine, msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza, Ashraf al-Qidra jana Ijumaa alitangaza habari ya kuaga dunia Mpalestina kwa jina la Mohammad Salem Sawarka kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya ndege za utawala haramu wa Israel kushambulia makazi ya raia katika mji wa Deir al-Balah.

Habari zaidi zinasema kuwa, Sawarka ni Mpalestina wa tisa wa familia moja kuuawa katika mashambulizi hayo ya kikatili ya jeshi la Israel dhidi ya makazi ya raia katika Ukanda wa Gaza. Shambulizi hilo dhidi ya makazi ya familia ya Rasmi Abu Malhous limesababisha pa watu 11 wa familia hiyo aghalabu yao wakiwa watoto wadogo kujeruhiwa vibaya.