Wakazi wa New York waendeleza maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani
(last modified Sat, 06 Jun 2020 17:16:39 GMT )
Jun 06, 2020 17:16 UTC
  • Wakazi wa New York waendeleza maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani

Wakazi wa New York nchini Marekani wameendeleza maandamano ya kupinga ubaguzi na ukatili wa polisi ya nchi hiyo dhidi ya watu weusi.

Katika maandamano hayo washiriki sambamba na kufanya maandamano katika mitaa ya mji wa New York na kukusanyika karibu na kituo cha polisi cha Brooklyn mjini hapo, walipiga nara za 'Maisha ya watu weusi yana thamani.' Inaelezwa kwamba kituo hicho kimegeuka na kuwa eneo la ukandamizaji wa polisi dhidi ya waandamanji wanaopinga ubaguzi nchini humo. Jumatano iliyopita mmoja wa watu wanaoshikiliwa katika kituo hicho mwenye umri wa miaka 35 kwa jina la Jamal Floyd alifariki dunia baada ya kupatwa na shambulio la moyo kufuatia afisa wa polisi kumpulizia kimiminika cha pilipili mtu huyo.

Ukandamizaji usio na kifani wa polisi wa Marekani katika kuwakandamiza waandamanaji

Katika siku za hivi karibuni miji mingi ya Marekani hususan Minneapolis jimbo la Minnesota imegeuka na kuwa ulingo wa maandamano makubwa ya wananchi wanaopinga vitendo vya ubaguzi na ukatili wa kuchupa mipaka wa polisi ya nchi hiyo. Tarehe 25 Mei Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu alimuua kinyama George Floyd, Mmarekani mweusi baada ya kumfinya shingoni kwa goti la mguu wake wa kushoto hadi alipopoteza maisha. Hatua hiyo iliibua hasira kali ya raia wa Marekani ambao walifanya maandamano makubwa nchini humo. Hata hivyo polisi walitumia mtutu wa bunduki kukabiliana na waandamanaji kitendo ambacho kimekosolewa vikali na wanasiasa wengi wa nchi hiyo.

Tags