Msimamo wa Macron dhidi ya uingiliaji wa Uturuki Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61771-msimamo_wa_macron_dhidi_ya_uingiliaji_wa_uturuki_libya
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa uingiliaji kijeshi wa Ufaransa nchini Libya ni mchezo hatari.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 23, 2020 07:34 UTC
  • Msimamo wa Macron dhidi ya uingiliaji wa Uturuki Libya

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa uingiliaji kijeshi wa Ufaransa nchini Libya ni mchezo hatari.

Kwa muhibu wa televisheni ya France 24, Rais Macron alisema hana Jumatatu baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na rais mwenzake wa Tunisia mjini Paris, Kais Saied, kwamba nafasi ya Uturuki huko Libya inahatarisha maslahi ya nchi hiyo, majirani zake, eneo zima na ya nchi za Ulaya.

Uturuki inaiunga mkono rasmi serikali ya Fayez Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Mapatano ya Kitaifa ya Libya dhidi ya hujuma ya kundi linalojiita Jeshi la Kitaifa la Libya ambalo linaoongozwa na jenerali muasi wa nchi hiyo Khalifa Haftar.

Khalifa Haftar

Novemba 27 mwaka uliopita Uturuki ilitiliana saini na serikali hiyo ya Libya ambayo inatambuliwa rasmi kimataifa, mapatano ya ushirikiano wa kiusalama na uchoraji mipaka ya baharini ili ipate kuchimba na kunufaika na maliasili ya nishati katika Bahari ya Meditarenea.

Hatua ya askari wa Haftar ya kuanzisha hujuma ya kijeshi kwa ajili ya kuuteka mji mkuu wa Libya Tripoli, mwezi Aprili 2019 na harakati za Serikali ya Mapatano ya Kitaifa GNA za kuulinda mji huo pamoja na kuwafukuza askari wa Haftar kutoka maeneo yaliyo karibu na mji huo, zimeshadidisha mapigano na kuvuruga kabisa uthabiti wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.