Ramaphosa: Afrika Kusini inakabiliwa na 'janga' la dhulma dhidi ya wanawake
(last modified Tue, 23 Nov 2021 07:27:54 GMT )
Nov 23, 2021 07:27 UTC
  • Ramaphosa: Afrika Kusini inakabiliwa na 'janga' la dhulma dhidi ya wanawake

Rais wa Afrika Kusini amesema dhulma za kijinsia na ukandamizaji unaofanywa na wanaume dhidi ya wanawake ni 'janga' la pili linaloisumbua nchi hiyo kwa sasa, mbali na tandavu ya ugonjwa wa Covid-19.

Cyril Ramaphosa alisema hayo jana Jumatatu na kusisitiza kuwa, wanaume wanapaswa kuungana kuhakikisha kuwa Dhulma za Kijinsia (GBV) zinamalizwa kikamilifu nchini humo.

Amesema takwimu mpya za Jeshi la Polisi la Afrika Kusini zimeonyesha kuweko ongezeko la kesi za ubakaji, ugomvi wa kinyumbani, na kinachosikitisha zaidi, ni mauaji ya watoto.

Takwimu zilizotolewa Ijumaa na polisi ya Afrika Kusini zinaonesha kuwa, visa vya ubakaji vilivyonakiliwa hadi sasa ni 9,556, yaani kesi mpya 634, sawa na ongezeko la asilimia 7.1 katika kipindi cha kati ya Julai na Septemba mwaka huu.

Novemba 25, Siku ya kulaani dhulma dhidi ya wanawake

Rais wa Afrika Kusini ameeleza kuwa, kati ya kesi 73,000 za hujuma zilizonakiliwa katika muda huo, zaidi ya 13,000 zinahusiana na ugomvi wa kinyumbani.

Ramaphosa amesema takwimu hizo zinafedhehesha, na kwamba dhulma hizo za kijinsia haswa dhidi ya wanawake ni janga la pili linaloisumbua Afrika Kusini, lakini kwa ushirikiana kama ilivyo katika janga la Corona, linaweza kuangamizwa.

 

Tags