Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aelekea New York
(last modified Mon, 18 Apr 2016 07:18:44 GMT )
Apr 18, 2016 07:18 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aelekea New York

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran leo asbuhi ameelekea mjini New York Marekani kwa ajili ya kushiriki katika sherehe za kutiwa saini makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia- Nchi katika Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa muafaka uliofikiwa mjini Paris Ufaransa.

Muhammad Javad Zarif atakuwa na mazungumzo pia na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na baadhi ya viongozi watakaohudhuria kwenye marasimu hayo, mbali na kushiriki kwenye marasimu hiyo ya utiaji saini makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia-Nchi.

Mashauriano ya Kerry na Zarif huko New York yatahusu utekelezaji wa Mpango wa JCPOA. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran vile vile atahutubia hadhara ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Havard katika ziara yake mjini New York.

Tags