Wapalestina 200 wameuawa shahidi Gaza katika masaa kadhaa yaliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105914-wapalestina_200_wameuawa_shahidi_gaza_katika_masaa_kadhaa_yaliyopita
Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imetangaza kuwa Wapalestina zaidi ya 200 wameuawa shahidi huko katika Ukanda wa Gaza katika masaa kadhaa yaliyopita.
(last modified 2023-12-12T08:29:59+00:00 )
Dec 12, 2023 08:29 UTC
  • Wapalestina 200 wameuawa shahidi Gaza katika masaa kadhaa yaliyopita

Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imetangaza kuwa Wapalestina zaidi ya 200 wameuawa shahidi huko katika Ukanda wa Gaza katika masaa kadhaa yaliyopita.

Marwan Al-Hams Mkurugenzi wa hospitali ya Youssef al-Najjar huko Gaza amesema: Ugonjwa wa ndui umeenea miongoni mwa watoto, karibu wagonjwa 1,500 hutembelea hospitali hiyo kila siku kufuatia kuongezeka tatizo la utapiamlo.  

Ripoti zinasema kuwa, hospitali za Ukanda wa Gaza zinakabiliwa na matatizo mengi kwa kukosa vifaa tiba katika kufanya upasuaji mbalimbali. Wafanyakazi wa tiba katika hospitali ya Shifa wanafanya kila wawezalo ili kuhuisha kitengo cha dharura cha kuwahudumia wagonjwa. Wakati huo huo mapema leo vyombo vya habari vilitangaza kuhusu kusikika sauti za milipuko karibu na hospitali ya al Shifa huko Gaza. 

Hospitali ya al Shifa, Ukanda wa Gaza 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, karibu watu elfu 20 wamekimbilia hospitali ya al Shifa na katika viunga vyake kwa ajili ya hifadhi. Hii ni katika hali ambayo hospitali za  Kamal Adwan na Al-Awda kaskazini mwa Gaza bado ziko chini ya mzingiro.