Nasrallah ampongeza kamanda wa Hizbullah aliyeuawa Syria
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah amempongeza kamanda mwandamizi wa harakati hiyo ya muqawama, Shahidi Mustafa Badreddine aliyeuawa Syria wiki jana na kusema alikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Israel.
Akizungumza katika khitma ya kamanda huyo hii leo mjini Beirut, Sayyed Nasrallah amesema, "Badreddine alikuwa na nafasi muhimu akiwa na shahidi Imad Mughniyeh…katika vita vya mwaka 2006 dhidi ya Israel kabla ya kuchukua majukumu kadhaa ikiwa ni pamoja na kusambaratisha mitandao ya kijasusi ya Israel."
Aidha amesema Badreddine alikuwa na jukumu la kusimamia vikosi vya kijeshi na kiusalama vya
Wapiganaji wa Hizbullah wanaoshirikiana na jeshi la Syria katika kupambana na makundi kadhaa ya kigaidi nchini humo wakiwemo magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh na Al Nusra.
Sayyed Nasrallah amesema, Badreddine akiwa nchini Syria alikuwa na nafasi muhimu sana kuzuia serikali ya nchi hiyo isiangukue mikononi mwa 'wakufurishaji na mabwana zao Wamarekani pamoja na majasusi katika eneo."
Kamanda huyo wa Hizbullah aliyekuwa na umri wa miaka 55 aliongoza tawi la Hizbullah lililokuwa linaisaidia serikali ya Syria katika vita dhidi ya magaidi. Aidha aliongoza oparesheni dhidi ya wanajeshi vamizi wa Israeli huko Lebanon na hivyo amekuwa akilengwa kuuawa kwa muda mrefu na Marekani, Israeli na waitifaki wao.
Shahidi Badreddine alikuwa binamu yake Imad Mughniyeh ambaye naye aliuawa shahidi katika oparesheni iliyotekelezwa na utawala haramu wa Israel mjini Damascus, Syria mwaka 2008.