-
Syria yasisitiza kuunga mkono kadhia ya Palestina
Jul 30, 2023 04:33Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imesisitiza juu ya misingi na misimamo yake thabiti na isiyoteereka ya kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina ambalo ardhi yake inakabiliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
Nasrallah: Waislamu wako tayari kuutetea Uislamu na Qur’ani Tukufu
Jul 30, 2023 01:18Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema jamii za Kiislamu haziwezi kustahamili kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, akisisitiza kwamba Waislamu wako tayari kikamilifu kuchukua hatua za kuwajibika kuulinda Uislamu na kitabu chao kitakatifu.
-
UN: Israel imebomoa majengo 54 ya Wapalestina mwezi Julai
Jul 30, 2023 01:07Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa vikosi vya kijeshi vya utawala haramu wa Israel vilibomoa majengo 54 yanayomilikiwa na Wapalestina huko Al-Quds (Jerusalem) Mashariki katika tarafa kubwa zaidi ya eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu mwezi Julai.
-
Wanajeshi Wazayuni: Netanyahu anaiteketeza kwa moto Israel
Jul 29, 2023 07:14Wanajeshi 1,300 wa utawala wa Kizayuni wamemshambulia vikali Benjamin Netanyahu na kusema kuwa waziri mkuu huyo wa Israel yuko tayari utawala wote wa Kizayuni uteketee kwa moto ili yeye binafsi aokoke.
-
Pango la Simba: Tutafanya operesheni nyingi zaidi dhidi ya Israel
Jul 29, 2023 06:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina ya Arin al Usud (Pango la Simba) imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba ujiandae kupokea vipigo vikali zaidi kutoka kundi hilo la mapambano.
-
Miripuko katika Haram ya Bibi Zainab SA Syria wakati wa maombolezo ya Imam Husain AS
Jul 29, 2023 06:00Juzi tarehe 27 Julai kulitokea mripuko mwingine wa kigaidi kwenye Haram ya Bibi Zainab SA mjini Damascus Syria ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha saa 48. Waislamu 6 waliuawa shahidi na wengine 23 kujeruhiwa kwenye shambulio hilo la kigaidi.
-
Hamas: Utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuibua vita vya kidini
Jul 29, 2023 04:27Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa mashambulizi ya Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa kwa mara nyingine tena yameonyesha namna adui alivyokusudia kutangaza vita vya kidini dhidi ya al Aqsa.
-
Nasrullah: Wimbi la Muqawama katika eneo lingali liko hai
Jul 28, 2023 04:36Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika hotuba aliyotoa usiku wa Ashura ya Imamu Hussein mjini Beirut kuwa: Tajiriba ya Muqawama nchini Lebanon imeonyesha kuwa wimbi la muqawama katika eneo lingali liko hai.
-
Jeshi la Israel lakiri lilishindwa katika operesheni ya kijeshi liliyofanya Jenin hivi karibuni
Jul 28, 2023 04:18Duru za kijeshi za Kizayuni zimekiri kushindwa operesheni ya hivi karibuni ya kijeshi iliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa Jenin na kambi yake ya wakimbizi.
-
Wapalestina 42 waliuawa katika uvamizi wa Israel kwenye kambi za wakimbizi mwaka 2023:
Jul 27, 2023 04:39Utawala haramu wa Israel umeongeza ukatili wake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuua Wapalestina 42 katika mashambulizi yake dhidi ya kambi za wakimbizi tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ripoti mpya inasema.