Serikali ya Uingereza kukabiliana na wahamiaji
https://parstoday.ir/sw/news/world-i16828-serikali_ya_uingereza_kukabiliana_na_wahamiaji
Wizara ya Biashara ya Kimataifa ya Uingereza imeweka wazi mpango wake wa kukabiliana na wahamiaji wanaoingia nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2016 01:11 UTC
  • Serikali ya Uingereza kukabiliana na wahamiaji

Wizara ya Biashara ya Kimataifa ya Uingereza imeweka wazi mpango wake wa kukabiliana na wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Liam Fox Waziri wa Uingereza anayehusika na Biashara ya Kimataifa amesema pambizoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Chama cha Conservative cha nchini humo huko Birmingham kuwa  nchi yake haiwakaribishi wahamiaji wanaowasili nchini humo na kutumia utajiri wa nchi.

Chama cha Conservative cha Uingereza katika mkutano wake wa kila mwaka

Waziri wa Biashara ya Kimataifa wa Uingereza ameongeza kuwa watu ambao watawasili Uingereza na kuishi bila ya kuzalisha chochote watatozwa fidia.

Liam Fox ameendelea kubainisha kuwa, wanamkaribisha mtu yoyote atakayeingia Uingereza na kusaidia kuzidisha utajiri wa nchi.

Utafiti uliofanywa na Akademia ya Uchumi ya London na kuchapishwa mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016, umeonyesha kuwa watu wanaohajiri katika nchi za Umoja wa Ulaya hawajasababisha  taathira hasi kwa mishahara, kazi na huduma za jamii za Uingereza. Hadi sasa Uingereza bado haijaamua ichukue siasa zipi kuhusu wahamiaji baada ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.