Wamarekani waendeleza maandamo dhidi ya Trump licha ya onyo kali la serikali dhidi yao
(last modified Thu, 26 Jan 2017 07:26:50 GMT )
Jan 26, 2017 07:26 UTC
  • Wamarekani waendeleza maandamo dhidi ya Trump licha ya onyo kali la serikali dhidi yao

Mamia ya wakazi wa jiji la New York Marekani wamemiminika mabarabarani katika kutangaza upinzani wao dhidi ya hatua za rais mpya wa nchi hiyo, Donald Trump.

Wakati rais huyo akiendelea na mchakato wake kwa ajili ya kuanzishwa ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico, mamia ya wakazi wa mji wa New York wameandamana kupinga  siasa za chuki sanjari na kutangaza uungaji mkono wao kwa wahajiri. Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na jumbe za kuwaunga mkono wahajiri Waislamu na pia wakimbizi wa Syria kwenda Marekani.

Waandamanaji dhidi ya Trump

Kadhalika waandamanaji wametoa jumbe zinazosema kuwa, haifai Wamarekani Waislamu wajihisi kutengwa au kufanyiwa miamala mibaya. Baadhi ya waandamanaji wameviambia vyombo vya habari kwamba, tangu rais huyo aiingie madarakani nchini humo, kumeshuhudiwa ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu na kwamba hali hiyo imetokana na serikali kudhibitiwa na watu wabaguzi na wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Polisi wakiwazuia waandamanaji

Maandamano dhidi ya Rais Donald Trump, yanafanyika katika hali ambayo hivi karibuni viongozi wa Marekani wamesema kuwa, kuanzia sasa wapinzani wanaoandamana dhidi ya rais huyo mpya watafungwa miaka 10 jela au kulipa faini kubwa kwa madai ya kufanya machafuko na uasi nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sasa waandamanaji hao watafungwa kifungo cha miaka 10 au kulipa  faini ya Dola elfu 25 za Kimarekani kila mmoja.

Tags