Trump akutana na Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57573-trump_akutana_na_rais_ashraf_ghani_wa_afghanistan
Katika safari yake ya ghafla nchini Afghanistan, Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 29, 2019 07:44 UTC
  • Trump akutana na Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan

Katika safari yake ya ghafla nchini Afghanistan, Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo.

Katika mazungumzo yao, Trump ametoa amri ya kuanza upya mazungumzo ya amani kati ya nchi yake na kundi la Taleban. Mazungumzo kati ya Marekani na kundi la Taleban yalisimama baada ya kuuawa askari mmoja wa Kimarekani mwezi Septemba mwaka huu. Rais Donald Trump pia amesisitiza juu ya kupunguzwa idadi ya askari wa Marekani nchini Afghanistan. Trump aliwasili Afghanistan jana usiku katika safari ambayo ilikuwa haijatangazwa kwa ajili ya kukutana na askari wa nchi yake. Akiwa nchini humo rais huyo ametembelea kambi ya jeshi la Marekani ya Bagram, ambayo ni kambi kubwa zaidi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Trump akizungumzo na askari wa Marekani nchini Afghanistan

Kuongezeka machafuko na harakati za makundi ya kigaidi nchini Afghanistan kunajiri katika hali ambayo tangu mwaka 2001 Marekani iliivamia kijeshi nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha usalama ndani ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti za viongozi wa serikali ya Kabul, uwepo wa askari wa kigeni wanaoongozwa na Marekani nchini humo, ndio umepelekea kuongezeka ukosefu wa usalama, kuongezeka makundi ya kigaidi pamoja na uzalishaji wa madawa ya kulevya.