-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuitembelea Misri karibuni
Jan 22, 2024 12:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian anataziwa kuitembelea Misri ndani ya siku chache zijazo, huku utawala wa Kizayuni ukiingiwa na kiwewe kutokana na kuendelea kuimarika uhusiano wa Tehran na Cairo.
-
Raisi: Iran inaunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel ICJ
Jan 22, 2024 07:31Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono uamuzi wa 'busara' na wa 'kihistoria' wa Afrika Kusini wa kuwasilisha kesi dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kuhusu jinai za mauaji ya kimbari zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Kikao cha leo cha wakuu wa NAM Uganda; Iran yataka jumuiya hiyo itilie mkazo kuihami Palestina
Jan 19, 2024 07:38Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM unafanyika leo katika mji mkuu wa Uganda, Kamapala huku Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwataka wanachama wa jumuiya hiyo kutilia mkazo uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran kushiriki mkutano wa NAM Uganda
Jan 19, 2024 03:31Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kwenda Kampala, mji mkuu wa Uganda kuhudhuria Mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM).
-
Wananchi wa Nigeria na Ghana wamuenzi Luteni Jenerali Qassim Suleimani + Video na Picha
Jan 08, 2024 03:48Kumbukumbu za kutimia mwaka wa nne tangu kuuliwa shahidi Luteni jenerali Shahidi Qassim Suleiman zimefanyika katika miji mikuu ya Nigeria na Ghana yaani huko Abuja na Accra kwa kuhudhuriwa na Waislamau wa matabaka mbalimbali na wafuasi wa kamanda huyo.
-
"Iran na Misri kuhuisha uhusiano wao wa kidiplomasia karibuni"
Dec 30, 2023 12:09Afisa wa ngazi za juu wa Misri amesema nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na Iran zinatazamiwa kufufua kikamilifu uhusiano wa pande mbili wa kidiplomasia, na hata kubadilishana mabalozi.
-
Mazungumzo ya kwanza ya simu baina ya Marais wa Iran na Misri; hatua ya kukuza uhusiano
Dec 24, 2023 08:14Jana Jumamosi, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alizungumza kwa simu na Rais Abdel Fattah El Sisi wa Misri, ikiwa ni mara ya kwanza kwa marais wa nchi hizi mbili kuzungumza kwa simu na ikiwa ni katika sehemu ya juhudi za kufufua uhusiano wa pande mbili.
-
Marais wa Iran na Misri wahimiza kustawishwa uhusino wa nchi mbili katika nyuga zote
Dec 24, 2023 02:38Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kwa simu na rais mwenzake wa Misri na kutilia mkazo udharura wa kustawishwa uhusiano wa nchi hizi mbili katika nyuga tofauti.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran azungumza na waziri mwenzake wa Afrika Kusini, Ghaza maudhui kuu
Dec 21, 2023 03:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Afrika Kusini na kujadiliana naye masuala mbalimbali muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa na hasa vita vya Ghaza huko Palestina.
-
Ayatullah Ramezani: Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa mujahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu
Dec 20, 2023 15:28Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kusema kuwa, Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa Mujahid fi Sabilillah (mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu).